FAHAMU NJIA ZA KUANDAA MAZINGIRA YA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO.

                   Fahamu Uandaaji wa njia nzuri za mafanikio 

                   Mafanikio katika maisha huandaliwa mapema kabisaa na hayatokei kama bahati mbaya kwa mtu fulani bali huja ni kwasababu ya maandalizi mazuri ambayo mtu amejiwekea na maandalizi yanatakiwa kufanyika mapema sana yani wakati huu wa ujana,kwa ushauri ndugu zangu ujana ni bahati ambayo wengi tumezawadiwa lakini tukitazama kwenye matumizi tunautumia ujana wetu vibaya sana kwa mfano fikiria matajiri wakubwa Tanzania na Africa ambao ni Aliko Dangote,Mohammed dewji,said salim bakhresa,Reginald mengi wangefika walipo  kama wangezitumia nafasi za ujanawao vibaya jibu ni hapana basi tujenge urafiki mzuri kati ya ujana wetu na mafanikio katika maisha yetu.hizi ni njia tano za kuandaa mazingira mazuri ya mafanikio,
                1.kujiwekea malengo kwa kila mwenye nia ya kufanikiwa katika maisha lazima awe na malengo ambayo ni timilifu kwa mda Fulani mfano ndani ya mwaka unaweza jiwekea malengo ya kununua gari na hakikisha malengo yako yanakua timilifu kwamba kipato unacho pata inaweza kua kwa siku au mwezi je kuna uwezekano wa kutimiza malengo yako uliyo jiwekea basi ukifanikisha hili utafurahia maisha yako.
                 2.uadilifu katika kazi hii ina ambatana na heshima katika kazi ambayo unajihusisha nayo watu wengi wamekosa uadilifu na heshima katika kazi zao na kupelekea ugumu wa mafanikio katika maisha yao,kama wewe unauza maji na kwa siku unaingiza shilingi elfu mbili basi wewe ni tajiri mkubwa sana kwa sababu kwa wiki moja utaingiza shilingi 14000/= na kwa mwezi shilingi 56000/=ambayo utakua umeitunza taratibu kabisaa na kuwekeza kwenye miradi mingine.
                   3.Biashara ya hisa na umiliki wa account ya benki hii ni moja kati ya biashara nzuri ambayo watu waliofanikiwa kimaisha wanajihusisha nayo na kujitengenezea mamilion ya fedha kupitia hisa basi pesa yako hutumiwa na kampuni kwenye shughuli mbali mbali na kukulipa na faida yako kulingana na kiwango cha pesa na muda ulio wekedha na pili faida ya kuwa na account benki inakuandaa kama mjasiliamali kupata mikopo mbali mbali kwa ajili ya uendeshaji wa biashara zako mbali mbali.
                    4.punguza matumizi ya pesa yasiyo ya lazima Hapa ndo pana matatizo sana watu wanashindwa kujizui dhidi ya matumizi ya pesa chakushangaza kabisaa unakuta mtu kwa mwezi anaingiza kiasi cha shilingi laki tano lakini yote huisha kwenye matumizi mabovu mabovu tu bila kujihusisha angalau ata kwa asilimia chache kwenye msingi wa maendeleo hakikisha hutembei na pesa ovyo,usinunue vitu ambavyo ni kwaajili ya kujifurahisha mwenyewe pia achana na mambo ya promosheni zinazotolewa na makampuni mbali mbali ni wizi mtupu huwa wapo kibiashara ukifanya hivyo utapunguza matumizi ya pesa ovyo.
                     4.Jiwekee mahusiano ya kibiashara kati ya biashara yako na kampuni husika (partnership)inayo endana na biashara unayofanya ili wakati wa matatizo katika biashara yako uwe na sehemu sahihi ya kupata msaada na pia wakati wa faida uwe na mkono mrefu wa kuingiza pesa katika biashara yako.



Published by Haruni Peter
Visit www.lightfursa.blogspot.com for more information

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAANA YA NENO BIASHARA NA FURSA KUU TANO MUHIMU

TABIA TANO HATARISHI ZINAZOWEZA KUKUONDOA KATIKA NJIA YA MAFANIKIO