MAANA YA NENO BIASHARA NA FURSA KUU TANO MUHIMU

Maana yaneno biashara
          Biashara ni neno ambalo sio geni kwKhufumasikio ya watu wengi sana, wanafalsafa mbali mbali duniani na watambuzi wa mambo wanasema kwamba mwanzo yaani miaka ya nyuma wakati ule ambapo watu walikua wachache sana msingi wa biashara ulikua ni kuuza na kununua bidhaa hiyo ndio ilikua biashara ya miaka ya nyuma, lakin sasa ndani ya karne hii ya ishirini na moja watu wameongezeka dunia na ongezeko la watu duniani limepelekea kuongezeka kwa matatizo mbali mbali ikiwemo magonjwa, uchafuzi wa mazingira kwa njia mbali mbali,ukosefu wa ajira, kuongezeka kwa uhalifu katika jamii n.k sasa biashara ya karne hii ni tofauti na mwanzo kwasababu unapochukua hatua ya utatuzi wa matatizo yaliyopo katika jamii yetu basi utalipwa pesa na watu wanaokuzunguka basi msingi wa biashara ya sasa umesimama katika nguzo ya utatuzi wa matatizo yaliyopo katika  jamii yetu.
Tuone mifano ya watu waliofanikiwa kwa kuchukua hatua ya utatuzi wa matatizo katika jamii.
            1.ndani ya sekta ya ulinzi kampuni iliyojitwaliya umaarufu mkubwa sana ndani ya East Africa kwa kutoa askari wa zuri na ubora wake katika suala zima la ulinzi inayo tambulika kama SGA(security guard) ,miaka arobaini iliyo pita mwanzilishi wa kampuni ya security guard aliona fursa katika jamii kwamba kunatatizo la ongezeko la uhalifu basi yeye hakulaumu Bali aliita kama nafasi yake yakuanzisha biashara nzuri sasa leo ni kampuni kubwa East Africa iliyo ajiri watu zaidi ya 17,000.
              2.pia tukitazama kwa umakini ndani ya sekta ya afya tunakutana pia na magonjwa mbali mbali sugu ambayo yanasumbua watu wengi sana ndani ya Tanzania ngoja tuipatie nafasi foreplan clinic ikiwa chini ya Dr. Mwaka ambayo imejipatia umaarufu mkubwa kwa utiaji wa tiba mbadala za asili pia Dr. Mwaka aliiona fursa kwamba Tanzania kuna watu wanahitaji huduma ya afya dhidi ya magonjwa mbali mbali ambayo yamekua kama kikwazo na matatizo kwako akachangamkia fursa sasa ni ameingiza pesa kubwa sana.

Fursa tano muhimu za kuzikazia macho kwa mjasiliamali.
                1.Biashara ya kilimo(agro business) Tanzania tumejaaliwa kuwa na ardhi ambayo inatoa fursa kwa madhao mbali mbali ya biashara lakini chakushangaza na kustajabisha watanzania wengi wanajihusisha na kilimo cha chakula wanazalisha kwa ajili ya chakula basi na tukiwekea mkazo katika nchi yetu katika swala la viwanda ndo sela kuu katika uongozi wa awamu ya tano na viwanda vinahitaji marighafi yakutosha kwa ajili ya kuzalisha zaidi.kama mjasiliamali mwenye shauku ya maendeleo basi tuchukue nafasi na kuwekeza katika kilimo cha biashara inalipa ndugu zangu usishangae amka simama na anza kutembea ushuhudie mambo makubwa.
                 2.Biashara ya usafirishaji inaweza kuwa usafirishaji wa bidhaa au abiria. Hii ni biashara ambayo inahitaji mtaji mkubwa kidogo ili uweze kua na faida kubwa sana ambapo itahitajika uwe na vyombo vya usafiri ambapo inaweza kuwa ni gari aina moja wapo kati ya zile za mizigo au abiria,ndege n.k tunaweza tazama mifano ya watu mbali mbali ambao wamewekeza katika biashara hii na kutengeneza kampuni kubwa sana hapa nchini kwa mfano fastjet  air ways,Rungwe express,new force .
                   3.Biashara ya vyombo vya habari na mawasiliano pia Tanzania kuna nafasi kubwa sana za kuwekeza kwenye vyombo vya habari na mawasiliano kwasababu ndani ya nchi yetu kuna vyombo vichache sana vya habari ndugu zangu kuna fursa hapa watu wengi hujawa na wasi wasi kwamba wanatengenezaje faida ndani ya vyombo hivi vya habari na mawasiliano faida hutengenezwa sana kupitia matangazo ambayo hurushwa na chombo husika kwa mfano mkataba wa matangazo huwa ni kwa dakika mbili mpaka tatu ambapo inaweza kua ndani ya wiki moja mbili au mwezi ndugu zanguni tuamke sasa tukimbie mbio za mafanikio.

             

                    4.Biashara ya kua wakala wa kuuza bidhaa za kampuni kwa sasa kampuni na viwanda vingi vimetengenezwa na watu wengi wenye nafasi za juu na kuna maeneo ambayo kwa hizo kampuni bado bidhaa zake hazijafika sasa kama mjasiliamali hii ni fursa kubwa ya kua wakala wa hiyo kampuni na kuuza bidhaa hizo kwasababu zitakua ngeni ndani ya hilo eneo na pia utapata faida ya kuuza bidhaa na kulipwa mshahara na kampuni, tumeona sana na kuota vingi sasa ni muda wa kusima na kufanya.
                    5.Biashara ya mtandao hii ni biashara ambayo inahitaji mtaji mdogo sana ambayo ni tofauti kabisaa na biashara zingine ambazo tumewai zifahamu kwasababu inamalipo mazuri sana kama mtu kama atawekeza vizuri mda wake na ataandaa vitu pendwa kwa wasomaji mbali mbali inaweza kua kuusu michezo, urembo na mitindo, biashara ,habari mbali mbali basi mtandao utakulipa kulingana na watu waliotembelea tofuti yako na matangazo mbali mbali ambayo yamerushwa kupitia tovuti iyoo.
   
   
Published by: haruni peter
Visit; www.light fursa.com for more information

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TABIA TANO HATARISHI ZINAZOWEZA KUKUONDOA KATIKA NJIA YA MAFANIKIO

FAHAMU NJIA ZA KUANDAA MAZINGIRA YA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO.