TABIA TANO HATARISHI ZINAZOWEZA KUKUONDOA KATIKA NJIA YA MAFANIKIO

                  Tabia tano hatarishi zinazoweza kukuondoa katika njia ya mafanikio
        Mafanikio katika maisha hutokana na mienendo ya kila siku ya mwanadamu kama mienendo yako sio sawa basi nafasi ya mafanikio ni ndogo sana  (nelson Mandela)na pia kuzaliwa maskini sio kosa lako Bali kufa angali maskini hilo ni kosa lako mwenyewe(bill gate),kitu ambacho kila mwanadamu anapaswa akitambue ni yeye ni nani nikimaanisha una talanta gani ,mungu kakuzawadia nini kama ni kipaji cha mziki, kama ni kipaji cha mpira, biashara ,mtaalamu wa urembo na mitindo mbali mbali,n.k ukisha jitambua inakupa urahisi wa kupata mafanikio kwasababu utawekeza nguvu yako yote kwenye kitu ambacho kipo ndani ya damu.
          Tukianza uchambuzi wa tabia moja baada ya nyingine kama mtu atatilia maanani na kuchukua hatua hakika ndugu yangu utafanikiwa,
         
              1.kutokujalibu, hili ni tatizo kubwa sana ambalo linatuweka mbali na njia ya mafanikio watu wengi ukiambiwa kuna fursa huchukui hatua ya kuitendea kazi na Bali tunabaki kuonyesha vikwazo kama wateja ntapata wapi na mtaji ni tatizo, ndugu zangu katika safari ya mafanikio kunavikwazo vingi sana ambavyo tunakumbana navyo na ushindi dhidi ya hivo vikwazo ndo mafanikio yako sasa tuache mazoea ya kupotezea mambo tuchukue hatua kwa mafanikio zaidi.
                2.uongo ,hili pia ni tatizo kubwa sana siku moja na kumbuka katika kipindi cha habari kutoka EAtv ambapo mahojiano yalikua dhidi ya Mohammad dewji ambapo aliongea dhahiri kwambo uaminifu ni kitu cha gharama kubwa sana ,ukiwa muongo basi utapoteza wateja wengi sana kwasababu wateja wetu huwa wanapashana habari na kuambiana mazuri na mabaya ya  mtu Fulani au bidhaa zake kwa mafanikio katika biashara yako inabidi uepukane na uongo.
                  3.kutokujifunza hili naweza kulitamka kama janga la kitaifa watanzania wengi hatuna utamaduni wakujisomea vitabu mbali mbali,kwenda katika matamasha mbali mbali ambayo hutoa mafunzo kuhusu vitu mbali mbali na katika hayo mafunzo ya matamasha na kujisomea vitabu ujuzi mbali mbali huongezwa kwa msomaji, tatizo linalotokea kwa watu ambao hawajisomei vitabu na kujihusisha kwenye matamasha mbali mbali ni kwamba utambuzi wa mambo mbali mbali huwa mdogo na hilo hupelekea ujuzi mdogo sana wa fursa zilizopo kalibu yako na utatuzi wa matatizo yanayoweza kukukabili,tunashauriwa kusima vitabu kwa faida yetu wenyewe ndugu zangu.
                   4.uvivu katika kazi kuwa na shauku  kubwa ya kufika sehemu Fulani bila kujishughulisha ni sawa na kusubiri moshi ufuke angali moto haujawashwa mafanikio huletwa na bidii yako mwenyewe hakuna msamalia mwema ambaye atajitokeza na kukupatia zawadi ya utajiri Bali utaipata kwa kujishughulisha sana uwezavyo pengine zaidi ya uwezo wako wa kawaida ,Fanya kazi kwa bidii sana mafanikio hufwata na kutafutwa kwa bidii zote kamwe hamna mtu anaye fatwa na mafanikio.
                    5.Anasa, starehe na utumbuaji wa Mali kupitiliza hiki kimekua chanzo kikubwa cha watu wengi kupotea katika njia ya mafanikio kuna watu wanaingiza pesa kidogo sana kwa mwezi lakini ukitazama Anasa starehe anazofanya zinapita ukubwa wa mshahara anaopata ndani ya mwezi mzima hatukatazi kufanya Bali tufanyej kwa kiasi.







  Published by:Haruni Peter
  Visit; www.light fursa.com for more information

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAANA YA NENO BIASHARA NA FURSA KUU TANO MUHIMU

FAHAMU NJIA ZA KUANDAA MAZINGIRA YA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO.